RB – Leipzig yaomba radhi kuwatimua uwanjani Wajapan kwa hofu ya virusi vya corona

In Kimataifa, Michezo

Klabu ya ligi kuu ya kandanda Ujerumani – RB Leipzig imeomba radhi kwa kikundi cha mashabiki wa Kijapan waliotimuliwa uwanjani kutokana na hofu ya virusi vya corona. Wageni hao waliambiwa waondoke uwanjani katika mchuano wa Jumapili wa ligi kuu nyumbani dhidi ya Bayer Leverkusen. Leipzig imesema kuwa walinzi wake walihitajika kufanya ukaguzi mkali dhidi ya vikundi au watu kutoka maeneo yanayozingatiwa kuwa kwenye kitisho kikubwa cha virusi hivyo. Klabu hiyo imekiri kufanya kosa na kuwa italirekebisha. Leipzig inapanga kuwaalika wageni hao wa Kijapan kwa mtanange wao ujao katika uwanja wa nyumbani. Klabu hiyo haikutoa maelezo zaidi ya tukio hilo. Hata hivyo shirika la habari la Ujerumani DPA limesema kikundi cha wageni 20 wa Kijapan waliambiwa waondoke uwanjani karibu dakika 10 kabla ya mchezo kuanza. Mechi hiyo ilikamilika kwa sare ya 1 – 1 na kuwaacha nambari mbili Leipzig wakiwa na pengo la pointi tatu nyuma ya vinara Bayern Munich.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WATANZANIA WATAKIWA KUIUNGA MKONO JKT QUEENS

MKUU wa JKT Meja Jenerali RAJABU MABELE, amewataka watanzania kuiunga mkono timu ya JKT Queens inayokwenda kuliwakilisha Taifa na

Read More...

SERIKALI YATOA BIL 424.6 UTEKELEZAJI MIRADI YA TANRODS RUKWA-ENG MWANGA

KATIKA kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu