SHEMEJI NI KIKWAZO KWA NYUMBA YANGU.

In Mahusiano

Wenzangu wote natumaini ni wazima leo nami naleta mada kwenye nzito nikitaka kusaidiwa mimi ni mwanaume na nimeoa, bahati mbaya baada ya kuoa wazazi wa mke wangu wote wakafariki akimuacha mke wangu na ndugu zake wa kike wawili ambao hawana kazi wa shule tegemeo lao ilikuwa mama yao na mke wangu dada yao.

Baada ya mama yao kufariki mke wangu akaniomba kama ndugu zake wangeweza kukaa nasi maana walikuwa hawana msaada nikakubali lakini baada ya muda hawa ndugu wa mke wangu naona wananifanyia mambo nisiyoelewa vituko kutwa haviishi ndani.

Ndugu yake mmoja amepata bwana basi yeye kutwa kwa huyo mwanaume hata na kurudi saa sita za usiku hata mimi mwenye nyumba nimeshalala na imetokea mara kwa mara nikimwambia mke wangu amkanye mdogo wake ananiambia kwanini ninawivu na mdogo wake ama namtaka mdogo wake? yani anakuwa mkali kabisa na wala hamwambii mdogo wake, huyu ndugu yake mwengine yeye ni mchafu sana, yani mpaka ananuka anaweza kukaa hata siku nne hajaoga tena akiwa kwenye hedhi ndio balaa ndani hapakaliki juzi kaniacha hoi baada ya kujisaidia haja kubwa kwenye ndoo ya jikoni na kuyaacha ndani.

Vituko vyao nimechoka sasa, nikimwambia mke wangu anasema nataka kuwafukuza wakati najuwa hawana pa kwenda, na inakuwa ugomvi kubwa sana na mke wangu mpaka nashindwa kuelewa ndugu zangu nifanye nini mwenzenu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WATANZANIA WATAKIWA KUIUNGA MKONO JKT QUEENS

MKUU wa JKT Meja Jenerali RAJABU MABELE, amewataka watanzania kuiunga mkono timu ya JKT Queens inayokwenda kuliwakilisha Taifa na

Read More...

SERIKALI YATOA BIL 424.6 UTEKELEZAJI MIRADI YA TANRODS RUKWA-ENG MWANGA

KATIKA kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu