DR CONGO yataka Rwanda iwajibishwe.

In Kimataifa

Jamhuri ya Kidemokrasi a Kongo imetishia kujiondoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iwapo jumuiya hiyo itashindwa kuiwajibisha Rwanda kwa madai ya unyanyasaji katika eneo la Mashariki lililokumbwa na ghasia.

Tishio hilo lilitolewa baada ya Mahakama ya Haki ya EAC kuripotiwa kukubali kuanza kesi dhidi ya Rwanda kuhusu kuhusika kwake na ghasia mashariki mwa DR Congo.

Naibu Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Samuel Mbemba aliutaja kuwa “ushindi wa mahakama kwa nchi yetu”.

Mbemba pia aliitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuanzisha uchunguzi kuhusu madai ya ukatili wa Rwanda mashariki mwa DR Congo.

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limekuwa likipambana na kundi la waasi la M23 – linalodaiwa kuuungwa mkono na Rwanda.

Taifa hilo la Afrika Mashariki limekuwa likipinga madai hayo ya Congo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Tanzania, Marekani zasaini makubaliano ya Dola Bilioni 3.14 kuimarisha sekta ya afya

Serikali za Tanzania na Serikali ya Marekani zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano katika sekta ya afya ya

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu