Ebola yazuka Kenya.

In Kimataifa

Mtu anayeshukiwa kuwa na Ebola amewekwa kizuini katika Hospitali ya Kericho, eneo la Bonde la Ufa kusini-magharibi mwa Kenya.

Mgonjwa huyo, ambaye ni mwanamke anaripotiwa kuwa na dalili zinazowapata wagonjwa wa Ebola.

Maafisa wa afya katika Kaunti ya Kericho wamesema kuwa alifanya safari kutoka Malaba eneo la mpaka kati ya Kenya na Uganda.

Hakuna ripoti yeyote iliyotolewa ya kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola, karibu na mpaka wa Malaba,Isipokuwa eneo la Magaharibi mwa Uganda.

Sampuli za damu za mgonjwa huyo zimechukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.

Matokeo ya awali ya vipimo yanatarajiwa kuwa tayari katika kipindi cha saa 12 mpaka 24.

Idara ya huduma za afya ya kaunti ya Kericho imesema inafuatilia kwa karibu suala hili na inafanya kazi pamoja na serikali kuu, kuhakikisha kuwa hatua madhubuti zinafuatwa kuhakikisha usalama wa kiafya kwa wengine.

Serikali ya Kaunti imeuhakikishia Umma kuwa hospitali ya kaunti ina uwezo na ina vifaa kuhakikisha mgonjwa anatengwa na kuwalinda watumiaji wengine wa hospitali, na imetoa wito kwa watu kuwa watulivu na wenye subira.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Tanzania, Marekani zasaini makubaliano ya Dola Bilioni 3.14 kuimarisha sekta ya afya

Serikali za Tanzania na Serikali ya Marekani zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano katika sekta ya afya ya

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu