EWURA yatangaza bei ya mafuta kupanda

In Uchumi

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji imetangaza ongezeko la bei kwa
mafuta yanayoingilia Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kushuka kwa thamani ya
Tsh dhidi ya Dola ya Marekani na ongezeko la bei katika soko la Dunia.

Lita moja ya Petroli imepanda kwa Tsh 20 huku Dizeli ikiongezeka kwa Tsh 74 na
Mafuta ya taa Tsh 44.
Ikilinganishwa na bei zilizokuwapo Januari 2020, bei za jumla ya Petroli imeongezeka
kwa Tsh 20.01 kwa lita, Dizeli imeongezeka Tsh 74.21 na Mafuta ya taa Tsh 43.96 kwa
lita moja.
Kanda ya Kaskazini inayopokea mafuta kupitia Bandari ya Tanga nako bei imepanda
ambapo bei ya rejareja ya Petroli imeongezeka kwa Tsh 42 kwa lita wakati Mafuta ya
taa yakipanda kwa Tsh 2 lakini Dizeli ikishuka kwa Tsh 18.

Bei ya jumla ya Petroli imeongezeka kwa Tsh 41.94 na Mafuta ya taa kwa Tsh 2.37 kwa
kila lita moja ikilinganishwa na bei za Januari huku dizeli ikishuka kwa Tsh 17.49.

Kanda ya Kusini inayojumuisha Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma bei za rejareja ya
Petroli imepanda kwa Tsh 35 wakati Dizeli ikishuka kwa Tsh 22. Ikilinganishwa na
Januari, bei ya jumla ya Petroli imepanda kwa Tsh 35.27 kwa lita

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKAGUA BARABARA YA SOMANGA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa asubuhi ya leo  Aprili 16, 2025 amewasili eneo la Somanga kukagua Miundombinu ya barabara kuu

Read More...

HATUTAWAACHIA CCM NAFASI TUTASHIRIKI UCHAGUZI MKUU – ACT WAZALENDO

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu amesema chama hicho kitashiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka

Read More...

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamohanga Afariki Dunia 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Gissima Nyamohanga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika ajali

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu