Kampuni ya teknolojia ya Google imewafuta kazi watumishi wake 48 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kutokana na madai ya unyanyasaji wa kingono. Watumishi hao ni pamoja na maafisa waandamizi 13. Afisa mtendaji mkuu wa Google Sundar Pichai amesema kwenye taarifa yake kwamba wamefanya mabadiliko mengi katika miaka ya hivi karibuni, ambayo ni pamoja na kuwa na msimamo mkali dhidi ya tabia zisizovumulika zinazofanywa na watu walio na madaraka. Utafiti huo ulioitwa “Elephant in the Valley” umebainisha kuwa takribani asilimia 90 ya wanawake wamesema wameshuhudia tabia za unyanyasaji wa kingono ofisini ama kwenye mikutano.
