Mke wa hayati #kobebryant aitwae #vanessabryant ametoa taarifa za kustaafishwa kwa jezi ya binti yake #giannabryant katika timu ya shule aliyokua akichezea enzi za uhai wake.
Jezi hiyo namba mbili #2 imestaafishwa rasmi shuleni hapo na haitokaa kuvaliwa na mtu yeyote kwa heshima ya binti huyo ambaye alikua na mchango mkubwa na nyota katika mchezo wa kikapu akifuata njia ya babaye.
Gianna na baba yake Kobe Bryant walifariki katika ajali ya ndege aina ya helkopta iliyotokea Jumapili ya January 26 huko California nchini Marekani.
Mke wa marehemu Kobe Bryant, Vanessa ameendelea kuomboleza vifo vya wapendwa wake hao kwa kuandika katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram
My Gianna, God I miss you! I’ve been so lucky to have woken up to see your gorgeous face and amazing smile for 13 year’s. Wish it would’ve been until my last breath. Mom love you to the moon and back, infinity plus 1 #2 #mambacita #gigibryant “.



