Waziri wa maliasili na utalii Dr Hamis Kigwangala amewaagiza maafisa wakuu wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na mamlaka nyingine kufanya kazi zao kwa uwadilifu ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria na ili kuweza kukuza na kuendeleza sekta ya utalii hapa nchini.
Ameyasema hayo wakati wa sherehe za uvishwaji vyeo vya jeshi USU kwa manaibu makamishna na makamishna wa hifadhi ya Ngorongoro iliyofanyika katika viwanja wa shule ya msingi Makao Mapya vilivyopo ndani ya hifadhi ya Ngorongoro
Amesema kuwa, amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa sheria ya jeshi USU ambayo taasisi nne ambazo ni TANAPA AMSA TFS na TAWA katika utekelezaji a majukumu yao kutoka mfumo wa kiraia uliokuwa umezoeleka hapo awali nma sasa kufuata mfumo wa Jeshi USU.
“Mfumo wa kuingia jeshi USU umelenga kutekeleza sheria ya wanyamapori no5 ya mwaka 2009 unaoelekeza kubadili mfumo wa uendeshaji kutoka wa kiraia na kuwa wa kijeshi ambao ulizinduliwa rasmi nov 17 mwaka 21019 na Mh. Makamu wa raisi Mama Samia Suluh Hassan ambapo hatua hii ni kutokana na changamato zilizokuwa zikijitokea kwa miaka ya hivi karibuni kama vile ujangili kwa wanyama, na uvamizi wa mifungo kwenye maeneo ya hifadhi”Alisema Kigwangala
Amesema serikali ya awamu ya tanu imedhamiria kuona kuwa sekta ya uhifadhi na ulinzi wa wanyamapori inaboreshqwa kiutendaji ili kukidhi matakwa ya kisheria na kuendana na mbinu za kisayansi na technologia na kuhakikisha maeneo yote yaliyotekwa kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori na uhifadhi yanalidwa kwa nguvu zote kwa kutoa matokeo chanya na endelevu kwa kuimarisha nidhamu, na ukakamavu uwajibikaji na uwadilifu illi kuongeza ubora katika utendajikazi kwa watumishi katika ulinzi wa rasilimali za taifa
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la wafugaji mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Pr, Abuid Kashamira amefanya zoezi la kuwatunuku vyeo viongozi hao ambapo amesema utekelezaji huo ni wa sheria no 5 ya mwaka 2009 ambapo ni kutoka mfumo wa kiraia kwenda jeshi USU ambayo italeta mabadiliko makubwa na yenye faida katika sekta ya utalii
Amesema kuwa,Vyeo hivyo ni muhimu kwa sababu ya maafisa na maaskari kutambuana, kujenga mtiririko sahihi wa Amri, kujenga nidham ya kijeshi, ukakamavu, ufanisi katika shughuli, na kuongeza na kujenga uzalendo katika kutekeleza majukumu na sheria za maliasili na utalii hapa nchini
Nae inspekta Jeneral Wa Polis Tanzania IGP Simon Siro amewapongeza makamishna hao kwa kupandishwa vyeo huku akiwataka kutumia vyeo hivyo vizuri na kufanya jeshi kuendelea kuheshimika na kuwa na nidhamu kwa kuzingatia kanuni na sheria
Hata hivyo sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali na waliopandishwa vyeo ni manaibu kamishna 2 ambao ni uhifadhi maendeleo ya jamii, huduma za shirika, na makamishna wahifadhi wasaidizi waandamizi wa idara mbalimbali za mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro




