Mbali na kulika, ndizi zina manufaa mengine, hasa katika urembo wa ngozi.
Ndizi zina virutubisho muhimu vinavyoboresha ngozi. Ndizi pia zina aina tatu za
sukari zinazojulikana kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’.
Hakikisha unanawa uso wako mara tatu kwa siku. Unapofanya hivyo unaondoa
uchafu.
Ndizi pia husaidia kuzuia chunusi.
Hakikisha unanawa uso kwa sabuni ambayo inaendana na ngozi yako. Ikiwa
ngozi yako ni ya mafuta, hakikisha unatumia sabuni ambayo itakuacha ukiwa
mkavu na kama ngozi yako ina ukavu, jioshe na sabuni itakayokufanya uwe na
unyevu.
Kulainisha ngozi
Changanya asali na ndizi moja iliyopondwa na upake kwenye uso na shingo.
Nawa uso kwa maji ya fufutende baada ya muda wa nusu saa. Fanya hivi angalau
mara moja kwa wiki.
Kung’arisha uso
Ndizi huwa na Vitamin C ambayo husaidia kuiweka ngozi kuonekana iking’aa.
Kwenye ndizi iliyopondwa, ongeza vijiko viwili vidogo vya juisi ya limau na upake
kwa uso na shingo. Osha kwa maji ya fufutende baada ya dakika 20. Ni vizuri
kupaka mchanganyiko huu wakati unapoenda kulala.
Kuzuia mikunjo
Ponda parachichi na ndizi pamoja. Paka kwa uso na uoshe baada ya muda.
Mchanganyiko huu hulainisha ngozi ya uso na kuwa laini lakini pia upunguza
ukubwa wa matundu ya ngozi ya uso wako.
Kusugulia uso (Scrubing)
Changanya ndizi na sukari kijiko kimoja, kisha paka usoni na usugue taratibu.
Ndizi hulainisha ngozi kavu na sukari huondoa seli zilizokufa kwenye ngozi.
Saga ndizi moja na Oats vijiko vitatu kisha changanya na asali na maziwa. Paka
usoni kwa dakika 15 kisha sugua.
