Mwili wa Baba mzazi wa Msanii wa Kizazi Kipya, Belle9 unatarajiwa Kuhifadhiwa leo huko nyumbani kwake Mkoani Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Manager wa Msanii huyo JAZ, amesema mzee huyo atazikwa leo kutokana na mwili wake Kuumia Vibaya.
“Ni kweli baba yake Belle 9 amefariki jana na mazishi ni leo saa nane kwasababu ameumia sana kwahiyo msiba hauwezi kukaa muda mrefu”Alisema JAZ wakati anaongea na kipindi cha FUNIKO BASE.
Marehemu Mzee, huyo alifariki usiku wa kuamkia jana baada ya kugongwa na Pikipiki iliyokuwa kwenye mwendo Kasi ambapo Pia Dereva wa Pikipiki hiyo naye aliumia Vibaya.
RADIO 5 TUNATOA POLE KWA BELLE9 NA MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA.
