Aliyekuwa Spika wa Bunge Job Ndugai, jana alihudhuria kikao
cha kwanza cha bunge la bajeti kwa mwaka 2022 tangu ajiuzulu.
Job Ndugai alijiuzulu wadhifa huo mnamo Januari 6 2022, kwa
maelezo ya kwamba alifanya hivyo kwa ajili ya maslahi ya
chama chake na Taifa, baada ya kuonekana akikejeli mkopo wa
Trilioni 1.3 uliochukuliwa na serikali.
Kupitia mitandao ya kijamii hivi karibuni, watu wengi walikuwa
wakihoji ni wapi alipo mbunge huyo wa Kongwa baada ya
kutoonekana kwa muda.
Jana amefika bungeni na kutambuishwa na spika wa sasa Dkt
Tulia Akson ambayo shangwe liliibuka toka kwa wabunge
wenzake.



