Klabu ya Tabora United itawakosa washambuliaji wake wawili Heritier Makambo na Yacouba Sogne kwenye Mechi Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Simba SC itakayochezwa Jumapili ya Feburuari 2.
Makambo atakosekana kwa sababu ya adhabu ya kadi tatu (3) za njano huku Sogne ataukosa mchezo huo kwa sababu ya majeraha.
Kwenye mchezo huo Tabora united wamepewa ahadi ya Milioni 50 endapo wakimfunga Mnyama.
