Venezuela kutoa mapipa milioni 50 ya mafuta kwa Marekani baada ya Maduro kuondolewa Madarakani

In Kimataifa

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Venezuela itatoa mapipa milioni 30 hadi 50 ya mafuta kwa Marekani, kufuatia operesheni ya kijeshi iliyomuondoa Rais Nicolás Maduro madarakani.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump alisema mafuta hayo yatakuwa ya ubora wa juu na yatauzwa kwa bei ya soko. Aliongeza kuwa mapato yatadhibitiwa na yeye binafsi kwa madhumuni ya kuwanufaisha wananchi wa Venezuela na Marekani.

Tamko hilo linakuja wakati Trump akidokeza kuwa sekta ya mafuta ya Marekani itaanza kufanya kazi nchini Venezuela ndani ya miezi 18, huku akitabiri uwekezaji mkubwa katika nchi hiyo. Hata hivyo, wachambuzi wanasema kurejesha uzalishaji wa mafuta wa Venezuela kwa viwango vya awali kunaweza kugharimu mabilioni ya dola na kuchukua hadi muongo mmoja.

Kauli ya Trump imetolewa siku moja baada ya Delcy Rodríguez kuapishwa kuwa rais wa mpito wa Venezuela. Rais wa zamani Nicolás Maduro yuko nchini Marekani akijibu mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya na umiliki haramu wa silaha.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Tanzania, Marekani zasaini makubaliano ya Dola Bilioni 3.14 kuimarisha sekta ya afya

Serikali za Tanzania na Serikali ya Marekani zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano katika sekta ya afya ya

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu