Warren asimamisha kampeni yake ya kuwania urais Marekani

In Kimataifa

Mwanasiasa Elizabeth Warren ametangaza kujiondoa kutoka kwenye mchuano wa kuwania kuteueliwa na chama cha Democratic kuwa mgombea wa kiti cha urais wa Marekani uliopangwa baadae mwaka huu.Warren mwenye umri wa miaka 70 na aliyewahi kuongoza kura za maoni kwenye kinyangányiro hicho, amefikia uamuzi huo baada ya kupata matokeo mabaya ya kura za mchujo kwenye majimbo kadhaa mapema wiki hii.Seneta huyo mpenda mageuzi wa Jimbo Massachusetts amesema anasitisha kampeni yake ya kuwania tiketi ya chama Democratic na kujizuia kutangaza mwanasiasa anayemuunga mkono kwenye mchuano huo.Wakati wa kura za mchujo kwenye majimbo 14 iliyofanyika siku ya Jumanne, Warren alishika nafasi ya tatu nyumba ya Seneta Bernie Sanders na makamu wa rais wa zamani Joe Biden

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WATANZANIA WATAKIWA KUIUNGA MKONO JKT QUEENS

MKUU wa JKT Meja Jenerali RAJABU MABELE, amewataka watanzania kuiunga mkono timu ya JKT Queens inayokwenda kuliwakilisha Taifa na

Read More...

SERIKALI YATOA BIL 424.6 UTEKELEZAJI MIRADI YA TANRODS RUKWA-ENG MWANGA

KATIKA kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu