Waziri Mkuu Kassim Majaliwa asubuhi ya leo Aprili 16, 2025 amewasili eneo la Somanga kukagua Miundombinu ya barabara kuu ya Dar es Salaam-Lindi ambayo imeathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
Mheshimiwa Waziri Mkuu ameambatana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stegomena Tax pamoja na Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega.Jana, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Amos Makalla aliwaambia wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Nanyamba mkoani Mtwara kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufika katika Daraja la Somanga leo, ili kuhakikisha mawasiliano yanarejea katika barabara ya kutoka Dar es Salaam kuelekea mikoa ya Kusini.
