Babu Tale Aachiwa.

In Burudani

MKURUGENZI wa Kampuni ya Tip Top Connection na Meneja wa Diamond Platnumz, Hamis Taletale maarufu Babutale ameachiwa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam tangu jana Alhamisi na sasa yupo uraiani japo haijafahamika iwapo yupo nje kwa dhamana au vinginevyo.

Tale alifikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar, juzi Jumatano Mei 23, 2018 kufuatia kesi yake anayodaiwa na Sheikh Hashim Mbonde kiasi cha Tsh. Milioni 250 ambapo kesi hiyo iliahirishwa baada ya hakimu aliyetoa amri ya kumkamata kutokuwepo mahakamani hapo.

Kipindi cha nyuma mahakama hiyo ilimwamuru Babu Tale alipe Sh. milioni 250 Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde, baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18, mwaka juzi, katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde aliyewalalamikia ndugu hao kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu