Harusi ya King Kiba yapata neema kubwa viongozi wa kiserikali nje na ndani wahudhuria

In Burudani
Usiku wa jana imefanyika sherehe nyingine ya harusi ya Alikiba na mkewe Aminah Rikesh Ahmed na mdogo wake Abdu Kiba na Ruwayda katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

Sherehe hiyo ilifaana zaidi baada ya kuhudhuriwa na watu lukuki wakiwemo wazazi wa wana ndoa wote na watu maarufu pamoja na viongozi wa serikali akiwemo mke wa rais wa awamu ya nne, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Àfya, Ummy Mwalimu, Naibu Waziri wa Kazi, Anthony Mavunde, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangalla na Gavana wa mji wa Mombosa, Hassan Joho ambaye pia ni mtu wa karibu wa msanii Kiba.


Mama Salma KKikwete (kushoto) akiwa na Waziri wa Àfya, Ummy Mwalimu

Katika sherehe hiyo Waziri Kigwangala amewataka maharusi wote kuchagua sehemu yoyote ya kitalii ndani ya Tanzania kwenda kufanyia fungate yao na yeye atagharamia kila kitu.

Lakini kubwa zaidi Alikiba alizindua kinywaji chake cha energy kinachoitwa Mofaya.


Waziri Kigwangalla akitoa neno kwa maharusi


Mama mzazi wa mke wa Alikiba (Aminah Rikesh Ahmed)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MO apatikana, atelekezwa na watekaji.

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema Bilionea/Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji ‘Mo’  aliyetekwa na watu wasiojulikana Oktoba 11,2018 amepatikana

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu