Jean-Pierre Bemba aachiwa huru kwa muda

In Kimataifa

Korti ya Kimataifa ya Uhalifu yenye makao yake mjini The Hague, ICC imemwachia kwa muda aliyekuwa Makamu Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jean-Pierre Bemba, baada ya kumuondolea hatia wiki iliyopita. Kuachiwa huko kwa muda kunafungamana na tuhuma za kuwahonga mashahidi wakati kesi yake ilipokuwa ikisikilizwa mwaka uliopita, ambayo kesi yake ya rufaa itasikilizwa tarehe 4 mwezi ujao wa Julai. Majaji wa mahakama ya ICC walimruhusu kuondoka katika jela ya mahakama hiyo mjini The Hague, ikiwa ataheshimu masharti magumu aliyowekewa. Mojawapo ya masharti hayo ni kuripoti mara moja kwenye vyombo vinavyohusika akitakiwa kufanya hivyo, kutobadilisha anuani yake bila kuiarifu mahakama, na kujizuia kutoa tangazo lolote hadharani. Wakili wa Bemba Peter Haynes amesema mteja wake ananuia kurejea mjini Brussels kujiunga na familia yake iliyoko huko.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mwanamfalme Saudia Kuchunguzwa kifo cha Khashoggi.

Kuna ushahidi kamili kwamba mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman na maafisa wengine wa ngazi za juu wanahusika kibinafsi

Read More...

Hafla ya kutambulisha tuzo ya serengeti yafanyika.

Waziri wa maliasilai na utalii Mh Hamis Kigwangala leo ameshiriki katika zoezi la utambulishwaji wa Tuzo ya Mbuga ya

Read More...

Serikali inadaiwa zaidi ya bilioni 6.

Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza kupitia Jeshi hilo limeiomba Serikali kuwalipa deni la shilingi Bilioni 6.45 fedha zilizotumika

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu