SABAYA AFIKISHWA MAHAKAMANI

In Kitaifa

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake 5 wafikishwa mahakamani kwa makosa matano ikiwemo uhujumu uchumi, kuongoza genge la uhalifu,Rushwa , utakatishaji fedha pamoja na unyang’anyi kwa kutumia silaha.

Mashtaka hayo yamesomwa mkurugenzi msaidizi katika ofisi ya taifa ya mashtaka anayeshughulika na usimamizi wa kesi Tumaini Kweka mbele ya Jaji Martha Mahumbuga hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya hakimu mkazi Arusha.

Kweka amesema kuwa upelelezi wa makosa yanayowahusisha kesi lengai ole sabaya na wenzake amesema ni tamati ya kuwafikisha mahakamani kutokana na kujiridhisha kwa mkurugenzi na kama Kuna makosa yatajidhihirisha yatapelekwa mahakamani.

Pia kweka amefafanua kuwa wamechelewesha kuwafikisha mahakamani kwasababu ya uchunguzi wa kina na Leo tumewaleta mahakamani kulingana na mashtaka waliyosomewa .

Hata hivyo mashtaka ya pili yamesomwa na Tarsila gervas mbele ya hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya arusha Salome mshasha amesema mtuhumiwa lengai ole sabaya, silvester nyagu pamoja Daniel Gabriel mbura wamesomewa kesi ya jinai ya uny’ang’anyi na utumiaji silaha .

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa ikiwepo ya uhujumu uchumi pamoja na kesi ya uny’ang’anyi ambapo imetajwa kusikilizwa tarehe 18/6 2021 .

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Waziri wa Uganda ajeruhiwa na mwanae kufa baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana

Watu wenye silaha wamemshambulia na kumjeruhi Waziri na Kamanda wa zamani wa jeshi la Uganda, na kumuua binti yake

Read More...

Ndugai Amtimua Bungeni Mbunge

Spika wa Bunge , Job Ndugai amemtimua bungeni mbunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuvaa suruali inayombana. Mbunge huyo

Read More...

Waziri wa Uganda apigwa risasi na watu wasiojulikana karibu na nyumba yake

Jenerali Katumba Wamala, Mkuu wa zamani wa Jeshi la Uganda na Waziri wa sasa wa Ujenzi na Uchukuzi amepigwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu