SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE.

In Michezo

Ombi la Barcelona la kumnunua kwa mkopo wa dau la £137m pamoja na kumpatia kandarasi ya kudumu mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, limekataliwa na PSG huku mabingwa hao wa ligue 1 wakiitisha dau la £229m. (Marca)

Manchester United imemfanya winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19, lengo lao kubwa katika uhamisho wa mwezi Januari na wanajiandaa kutoa dau la £100m. (Sun)

jadon sancho

Liverpool, Manchester City, Manchester United, Arsenal na Chelsea ni miongoni mwa klabu kuu barani Ulaya zinazomlenga mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 20, ambaye ana thamani ya £91m. (Sport1 – in German)#

Beki wa Liverpool na raia wa Croatia asiyehitajika sana Dejan Lovren, 30, anaivutia klabu ya Ujerumani ya Bayer Leverkusen baada ya kufeli kupata uhamisho kuelekea Roma. (Bild – in German)

Tottenham imeanza mazungumzo ya kumuuza kiungo wa kati wa Kenya Victor Wanyama, 28, kuelekea klabu ya Bruges kwa dau la £11m.

Victor Wanyama

Mshambuliaji wa Ubelgiji Michy Batshuayi, 25, anataka kusalia na kupigania nafasi yake Chelsea lakini ataitazama hali mwezi Januari. (Standard)

Manchester City inachunguza hali ya kiungo wa kati wa Argentina na klabu ya Velez Sarsfield Argentine Thiago Almada, 18, ambaye bado hajaandikisha upya kandarasi yake na klabu hiyo.. (A Bola, via Manchester Evening News)

Thiago Almada

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu