“SUKARI HAIWEZI KUTUFANYA MATEKA” – Mkenda

In Kitaifa

SERIKALI imeutaka uongozi wa kiwanda cha sukari Kilombero kuhakikisha inaharakisha mchakato wa uwekezaji ili kuongeza uwezo wake wa kuchakata miwa yote inayozalishwa na wakulima wadogo ili nchi ijitosheleze kwa sukari. Kauli hiyo ya serikali imetolewa jana na Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda wakati alipokutana na kuzungumza na Menejimenti ya Kampuni ya Sukari ya Kilombero pamoja na wakulima wa miwa wa wilaya ya Kilombero.

Profesa Mkenda alisikitishwa na taarifa ya Bodi ya Sukari kuonesha kuwa wastani wa tani 350,000 za miwa ya wakulima wadogo sawa na tani 35,000 za sukari endapo zingechakatwa hukosa kununuliwa na wamiliki wa viwanda vya kuchakata miwa vya Kilombero huku nchi ikiendelea kuwa na upungufu wa sukari.

“Hatuwezi kuwa mateka katika suala la uzalishaji sukari kwa kumtegemea mzalishaji mmoja. Tatizo wakulima wana miwa hainunuliwi na mwekezaji halafu nchi inaendelea kutoa vibali kwa mwekezaji kuagiza sukari nje ya nchi wakati anatakiwa kuongeza uwezo wa viwanda vyake kuchakata miwa ya wakulima,” alisema Waziri Mkenda. Akizungumza na wakulima wa miwa wa wilaya ya Kilombero kwenye ukumbi wa chuo cha Taifa cha Sukari (NSI) Waziri Mkenda alisikiliza kero za wakulima waliolalamikia kitendo cha mwekezaji Kampuni ya sukari Kilombero kushindwa kununua miwa yote takribani tani 800,000 inayozalishwa na wakulima ili kuchakata sukari.

Waziri huyo wa Kilimo alisema takwimu za uzalishaji miwa zinaonesha wastani wa tani 350,000 hazijanunuliwa na mwekezaji Kilombero Sugar Co. Ltd ambapo zingetosha kuzalisha sukari tani 35,000 kwa maana hiyo nchi ingeagiza nje sukari tani 5,000 pekee kati ya 40,000 za upungufu wa sasa. Kufuatia hali hiyo Profeda Mkenda aliagiza uongozi wa kiwanda hicho kuharikisha mchakato wake wa kuongeza uwezo wa kiwanda kuchakata miwa kutoka tani 629,000 mwaka 2018/2019 hadi kufikia tani 800,000 msimu huu ili miwa yote ya wakulima wadogo inayozalishwa sasa na kukosa soko itumike kuzalisha sukari.

Alibainisha mpango wa wizara yake kutaka suala la upungufu wa sukari kuisha ambapo amepongeza hatua zilizochukuliwa na Rais John Pombe Magufuli alipoingia madarakani mwaka 2015 kudhibiti uagizaji sukari toka nje ili kutoa fursa kwa wawekezaji wa ndani “Kabla Rais Magufuli hajaingia madarakani nchi ilikuwa ikiagiza sukari tani 125,000 toka nje lakini kutokana na hatua za udhibiti serikali imefanikiwa kupunguza uagizaji wa sukari hadi wastani wa tani 40,000 mwaka 2020 ili kutoa fursa kwa viwanda vya ndani kuzalisha “ alisema Waziri Mkenda.

kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero Balozi Mstaafu Ami Mpungwe alisema kiwanda hicho ni kielelezo kizuri cha faida ya ubinafishaji kutokana na kuongeza uwezo wa kuzalisha sukari kutoka tani 28,000 mwaka 1998 hadi tani 128,000 za sukari mwaka 2020 kwa viwanda vyote viwili ( Kilombero I na Kilombero II) “Kama kuna mtu ana fikra kuwa wakulima wadogo tunawadharau siyo kweli, tunawategemea sana ili viwanda vyetu viendelee na sasa tunalenga kufikia kununua miwa ya wakulima asilimia 60 baada ya upanuzi wa kiwanda mwaka 2023,” alisema Balozi Mpungwe.

Mmoja wa wakulima wa miwa Helina Kopa wa Kilombero akiongea kwenye mkutano huo alilalamikia kitendo cha kampuni kushindwa kununua miwa ya wakulima kwa kigezo kuwa imekaa muda mrefu baada ya kuvunwa huku akitaka serikali kuchunguza mwenendo wa uuzaji miwa unaofanywa na kampuni.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu