Marekani Yaishambulia Syria kwa Makombora

In Kimataifa

Marekani imefanya shambulizi la makombora takriban 50 ,yalipigwa katika kambi ya jeshi la anga mjini Homs nchini Syria.

Awali maafisa wa Marekani walisema wana mpango wa kuchukua hatua za kijeshi baada ya Syria kushutumiwa kutumia silaha za kemikali katika mji unaodhibitiwa na waasi, ambapo watu kadhaa wamepoteza maisha.

Mashambulizi hayo yametekelezwa kutoka kwenye meli za kijeshi za Marekani katika bahari ya Mediterranea.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema ameamuru kutekelezwa kwa mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Syria huku akitoa wito kwa mataifa yote yaliyostaarabika kukomesha vitendo vya mauaji na umwagaji damu nchini humo

Naye mshirika wa Syria Urusi ametahadharisha madhara yatokanayo na hatua zozote za kijeshi zinazochukuliwa na Marekani dhidi ya Syria .

Mike Pregent ni mchambuzi wa masuala ya mashariki ya kati ameiambia BBC kuwa mashambulizi hayo yametoa ujumbe mzito kwa Assad.

Shambulio hilo linawapa Watu wa Syria matumain, na ninachomaanisha ni kuwa haya hakika haya ni Mashambulizi dhidi ya vikosi vya anga vya Assad, silaha za kemikali, pengine dhidi ya hifadhi za mafuta halikadhalika.hivyo haikuwa dhidi ya raia, haikuwaweka marubani wa kimarekani hatarini. Ulikuwa ujumbe maalum kwa Assad kuwa usitumie jeshi lako la anga kuwaadhibu raia, hivyo nafikiri ni ujumbe wenye nguvu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WATANZANIA WATAKIWA KUIUNGA MKONO JKT QUEENS

MKUU wa JKT Meja Jenerali RAJABU MABELE, amewataka watanzania kuiunga mkono timu ya JKT Queens inayokwenda kuliwakilisha Taifa na

Read More...

SERIKALI YATOA BIL 424.6 UTEKELEZAJI MIRADI YA TANRODS RUKWA-ENG MWANGA

KATIKA kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu