Mbunge wa Jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima leo
amesimama bungeni kuchangia Bajeti ya Ofisi ya Waziri mkuu
na kueleza kuwa,hakuna taifa lililoendelea duniani bila mpango
wa muda mrefu.
Katika mchango wake Askofu Gwajima ameeleza kuwa kama
itatokea siku nchi ikapata Rais asie na maono basi taifa
litaanguki pua kwani hatakuwa na mpango wa kitaifa anaopaswa
kuufuata.



