Kabila Ahukumiwa Kifo na Mahakama ya Kijeshi DRC

In Kimataifa

Mahakama ya Kijeshi nchini Kongo (DRC) imemhukumu kifo Rais wa zamani Joseph Kabila kwa kukosa kuhudhuria kesi yake (in absentia), baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu wa kivita, uhaini na uhalifu dhidi ya binadamu.

Kesi hiyo inahusishwa na madai ya usaidizi wake kwa waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda mashariki mwa DRC. Jaji Mkuu wa Kijeshi, Luteni Jenerali Joseph Mutombo Katalayi, alisema Kabila ametiwa hatiani kwa makosa ya mauaji, ubakaji, mateso na uasi.

Kabila, aliyeongoza taifa kuanzia 2001 hadi 2019, amekanusha tuhuma na kudai mchakato wa kisheria umeingiliwa kisiasa. Mahakama pia imemwamuru kulipa fidia ya takribani dola bilioni 50 kwa serikali na waathiriwa.

Tuhuma dhidi ya Kabila zimeibua hofu ya kuongeza mgawanyiko nchini humo, hasa kutokana na mapigano ya muda mrefu mashariki mwa DRC ambapo waasi wa M23 sasa wanadhibiti maeneo makubwa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini.

Serikali ya Rais Félix Tshisekedi tayari imesitisha chama cha kisiasa cha Kabila na kuchukua mali za viongozi wake, huku Rwanda ikiendelea kukanusha kuhusika moja kwa moja katika vita hivyo.
#radio5fm

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

NIFFER NA CHAVALA WAACHIWA HURU NA MAHAKAMA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imewaachia huru leo mchana vijana Jennifer Jovin (26), maarufu kama

Read More...

Trump kukutana na viongozi wa Rwanda na DR Kongo Alhamisi

Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na viongozi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku ya Alhamisi

Read More...

SERIKALI YAAGIZWA KUFUTWA KWA LESENI 73.

Serikali kupitia Wizara ya Madini imeielekeza Tume ya Madini kufuta jumla ya leseni 73ambazo maeneo yake hayajaendelezwa. Hayo yameelezwa leo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu