Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt Maulid Madeni ameongoza
zoezi la kutoa mafunzo kwa waandikishaji wa wapiga kura
kwenye daftari lakudumu la uchaguzi unaotarajiwa kufanyika
mwaka huu 2020.
Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt Maulid Madeni amesema
kuwa ni utaratibu wa kawaida kutoa mafunzo hayo kila
unapokaribia uchaguzi lengo likiwa ni kuwapatia wasimamizi
hao ujuzi wa utekelezaji wa majukumu yao vizuri katika kipindi
cha uchaguzi.



