Baada ya Clatous Chota Chama kumaliza mkataba wake wa kuichezea Simba SC jana June 30, 2024, hatimaye ametambulishwa rasmi kama Mchezaji mpya wa Yanga SC na kumaliza tetesi za muda mrefu kwa Chama anaondoka Simba SC baada ya kuitumikia kwa miaka 6 katika vipindi viwili tofauti.

Chama alijiunga Simba SC kwa mara ya kwanza 2018 akitokea Lusaka Dynamos ya Zambia na kisha 2021 kuondoka Simba SC na kujiunga na RS Berkane aliyodumu kwa msimu mmoja na kurejea Simba SC 2022.



