Dkt Samia: Tutashirikiana kuendeleza matumizi nishati ya nyuklia

In Kitaifa

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ipo tayari kushirikiana na mataifa ya Afrika pamoja na taasisi za kimataifa kuendeleza matumizi ya nishati ya nyuklia ili kuimarisha usalama wa nishati na maendeleo ya muda mrefu barani Afrika.

Akizungumza katika Mkutano wa Ubunifu wa Nishati ya Nyuklia Afrika (NEISA 2026) uliofanyika Kigali nchini Rwanda Mei 19, 2026, Dkt Samia amesema mahitaji ya umeme yanaongezeka kwa kasi kutokana na ukuaji wa viwanda, miji na sekta mbalimbali za uchumi, hivyo nishati ya nyuklia ni moja ya suluhisho muhimu kwa mustakabali wa Afrika.

“Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi za Afrika, taasisi za kimataifa na sekta binafsi kuhakikisha nishati ya nyuklia inakuwa chachu ya ustawi na usalama wa nishati Afrika,” amesema Dkt Samia.

Mkutano huo uliwakutanisha viongozi wa sera, wataalamu wa nishati na wadau wa maendeleo kujadili namna ya kuharakisha matumizi ya nishati ya nyuklia kama chanzo salama na safi cha umeme kwa maendeleo ya uchumi wa Afrika.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu