MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

In Kitaifa

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya JKT kwa vijana wa Kundi la Mujibu wa Sheria, Operesheni Linda Amani, na Kundi la Kujitolea, Operesheni Nishati Safi.

Mafunzo hayo yamefungwa katika Kikosi cha Kanembwa JKT, Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, ikiwa ni hatua inayohitimisha rasmi mchakato wa mafunzo kwa vijana hao katika kambi mbalimbali nchini.

Ufungaji wa mafunzo katika kambi mbalimbali za JKT ulianza Septemba 8, 2026, ambapo sherehe zilifanyika kwa tarehe tofauti kulingana na ratiba ya kila kambi.

Katika baadhi ya kambi, Meja Jenerali Mabele aliwakilishwa na viongozi wengine wa JKT katika hafla za ufungaji, huku leo akiongoza mwenyewe hafla ya mwisho katika Kikosi cha Kanembwa.

JKT leo wanahitimisha rasmi mafunzo ya vijana wote waliokuwa katika kambi zote nchini na hafla ya Kakonko ni tukio la ujumla kwa niaba ya vikosi vyote vilivyokuwa vikiendesha mafunzo nchini.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Tanzania, Marekani zasaini makubaliano ya Dola Bilioni 3.14 kuimarisha sekta ya afya

Serikali za Tanzania na Serikali ya Marekani zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano katika sekta ya afya ya

Read More...

KIWANGO CHA KUJITEGEMEA KWA UCHUMI YAONGEZEKA

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, GERSON MSIGWA,

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu