FIFA yazitaka timu zitakazocheza Kombe la Dunia kuepuka malumbano ya kisiasa

In Kimataifa, Michezo

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, Gianni Infantino, ameziandikia barua nchi 32 zitakazoshiriki katika michezo ya Kombe la Dunia nchini Qatar, kujikita katika michuano hiyo badala ya kuiburuta kandanda katika mizozo ya kisiasa na kiitikadi. Infantino amesema katika barua hiyo kwamba kila mtu atakaribishwa nchini Qatar bila kujali asili yake, imani yake ya kidini, jinsia, utaifa au tabia yake ya kimapenzi.

Kituo cha habari cha Sky News cha nchini Uingereza ambacho kimepata nakala ya barua hiyo, kimesema haielezi chochote kuhusu ombi la nchi nane za Ulaya, ambazo zilitaka manahodha wa timu zao wavae utepe wenye mchanganyiko wa rangi unaowakilisha haki sawa kwa wapenzi wa jinsia moja, kama jibu kwa sheria za Qatar zinazokataza ushoga. Watetezi wa haki za binaadamu pia wanakosoa rekodi ya Qatar ya haki za binadamu, hususan mazingira duni kwa wafanyakazi waliojenga viwanja vya michezo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SERIKALI YATOA BIL 424.6 UTEKELEZAJI MIRADI YA TANRODS RUKWA-ENG MWANGA

KATIKA kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Read More...

Kasri la R. Kelly “Chocolate Factory” lauzwa Chicago Baada ya Historia ya Utata

Nyumba kubwa iliyoko katika suburbs za Chicago, maarufu kama “Chocolate Factory” ya R. Kelly kutokana na albamu aliyorekodi hapo,

Read More...

UJENZI WA DARAJA LA 6 KWA UREFU TANZANIA LA PANGANI WAFIKIA ASILIMIA 74.3

Ujenzi wa Daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525 na Barabara unganishi na mchepuko zenye urefu wa Kilomita

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu