Mwanamke mmoja nchini Uganda anayefahamika kwa jina la Ann Grace
Aguti, amewachukiza Wazazi, Viongozi wa Dini na Jamii yake baada ya kuwaoa
wanaume watatu na kumpa kila mmoja wao nyumba moja kati ya saba anazomiliki, kwa
sasa ana mimba na bado hajamtaja muhusika wa mimba hiyo.
“Baba mimi ni Mtu mzima ambaye nina maisha yangu ni haki yangu kuwa na
Wanaume watatu ambao wote wanaelewana bila ugomvi, ni nani kati yenu nyie
Viongozi wa Dini na hata wewe Baba atanifanya kuwa Mke, kama mtalazimisha
kuwafukuza Wanaume wangu watatu niliowaoa”-Ann baada ya Baba kutishia
kuwafukuza Wanaume wake.
“
Natamani kuwa na Mume atakayenihudumia kama Mke, ina raha yake ila
sijabatika, Mume wangu wa kwanza niliyezaa nae Watoto watatu alikuwa Marioo
nikamuacha kisa alizidisha wivu, nimewaoa hawa Wanaume watatu, nawalisha
nimewapa kila mmoja nyumba, ila bado natafuta Dume atakayeweza
kunigharamia anaweza hata kuwa Mume wa nne ”-Ann Grace



