Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape
Nnauye,ametahadharisha halmashauri zote nchini kuwa makini
na wenye Pesa ili wasitumie uwezo wao kununua majina ya
mitaa na barabara.
Waziri Nape amesema uwekaji wa majina ya mitaa na barabra ni
vyema yakaakisi uhalisia wa nchi,ikiwamo kutumia majina ya
viongozi mashuhuri wa nchi na majina ya baadhi ya watu
mashuhuri kwenye maeneo.
Waziri Nape ametoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na
viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro,katika mwendelezo wa ziara
yake ya kukagua na kuhamsisha zoezi la anwani za makazi.



