JCB Ailipua Media, “Hip Hop Inabaniwa Redioni, Wasanii Wachache Wapewa Nguvu Zote!”

In Burudani, Kitaifa

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini, JCB, anayetoka kundi la Watengwa, ameeleza wasiwasi wake kuhusu mwenendo wa tasnia ya muziki, akidai kuwa vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kudhoofisha ukuaji wa Hip Hop.

Akizungumza na Radio 5, JCB amesema pamoja na Hip Hop kuwa na ushawishi mkubwa kijamii na kielimu, bado haipati nafasi stahiki kwenye redio nyingi nchini. Amebainisha kuwa mzunguko wa nyimbo unaochezwa mara kwa mara unahusisha wasanii wachache tu, jambo linalobana fursa kwa aina nyingine za muziki hususan Hip Hop.

Kwa mujibu wa msanii huyo, hali ya sasa ya upangaji wa muziki redioni imejikita zaidi katika kuendeleza umaarufu wa wasanii wachache wa Bongo Flava, huku Hip Hop ikiachwa pembeni licha ya kuwa na mchango mkubwa katika kuelimisha na kuibua mijadala ya kijamii.

Aidha, JCB ameihusisha pia dhana ya utandawazi kama sababu inayochangia mabadiliko ya ladha ya muziki kwa wasikilizaji, hali inayosababisha kupungua kwa usikilizwaji wa Hip Hop ya ndani. Hata hivyo, amesisitiza kuwa vyombo vya habari vina nafasi muhimu ya kusawazisha hali hiyo kwa kutoa fursa sawa kwa wasanii wa mitindo mbalimbali.

Ameongeza kuwa iwapo Hip Hop ingepewa uzito sawa wa urushaji wa nyimbo kama ilivyo kwa wasanii wakubwa wanaotawala redio kwa sasa, basi ingeweza kufikia mafanikio makubwa zaidi na kupanua wigo wa ushawishi wake kwa jamii.

JCB ametoa wito kwa vyombo vya habari kubadilisha mtazamo na kuhakikisha kunakuwa na mchanganyiko mpana wa muziki redioni, ili kukuza tasnia kwa usawa na kutoa nafasi kwa vipaji vyote kujulikana.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Tanzania, Marekani zasaini makubaliano ya Dola Bilioni 3.14 kuimarisha sekta ya afya

Serikali za Tanzania na Serikali ya Marekani zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano katika sekta ya afya ya

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu