Kamati Kuu ya (CHADEMA) kuketi kesho.

In Kitaifa, Siasa
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kesho inakutana katika kikao cha ‘dharura’ jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar, Salum Mwalimu amesema lengo la kikao hicho ni kufanya tathmini ya hali ya kisiasa nchini.
Alipotakiwa kueleza kama lengo la kikao hicho ni kujadili ziara ya waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwenda Ikulu, Mwalimu amesema kikao hicho si cha dharura kwani kilipangwa kufanyika Desemba mwaka jana lakini kiliahirishwa kutokana na sikukuu za mwisho wa mwaka.
Amesema ajenda za kikao hicho zilipangwa kabla Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema hajaenda Ikulu hivyo hakina uhusiano na ziara hiyo ila huenda jambo hilo likajitokeza.
“Suala hilo halipo kwenye ajenda ila linaweza kujitokeza na likijitokeza litazungumziwa lisipojitokeza basi,” amesema Mwalimu na kuongeza;
 
“Hata hivyo kwa upande wake inaweza kuwa fursa nzuri kuielezea Kamati Kuu na viongozi wenzake nini kilitokea.”

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu