KIHONGOSI AWATAKA WANANCHI KUTORUHUSU MAKUNDI KUVURUGA AMANI.

In Kitaifa

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo, KENANI KIHONGOSI, amedai kuwa chama hicho kimepata taarifa zinazoonyesha kuwapo kwa vikao vya siri vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA kwa lengo la kuhamasisha maandamano na vurugu, huku akiwataka wananchi kutoruhusu makundi yoyote kuvuruga amani na utulivu wa nchi.

KIHONGOSI amesema hayo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ,ambapo mesema taarifa walizonazo zinaashiria kuwa baadhi ya wanasiasa pamoja na makundi ya wanaharakati wamekuwa wakiratibu ajenda za maandamano badala ya kushiriki katika mijadala ya maendeleo.

Amesema,kutokana na hali hiyo, amewataja viongozi wa CHADEMA akiwemo John Heche, Boniface Jacob na Godbless Lema, akiwataka kuelekeza nguvu zao katika ujenzi wa taifa kwa hoja na kushindana kwa sera badala ya kuhamasisha vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa wananchi.

Pia, KIHONGOSI amesisitiza kuwa CCM imeendelea kujikita katika kutatua changamoto za wananchi kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwemo afya, maji, elimu na miundombinu, akisema hicho ndicho chama kinachokipa kipaumbele.

Hata hivyo,amesema kuwà katika ziara mbalimbali zilizofanywa na CCM, viongozi wamekutana na wananchi kupitia mikutano ya hadhara na kusikiliza kero zao ili kupata majawabu ya changamoto zinazowakabili, huku akimpongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa uongozi anaousema umeleta maendeleo katika sekta mbalimbali.

Pia amewataka wananchi, wazalendo na wapenda maendeleo kutoshabikia maandamano na vurugu kwa namna yoyote ile, akisema matukio hayo mara nyingi huwaathiri wananchi wa kawaida zaidi kuliko viongozi wa kisiasa.

Amesema kuwa kuna watu walioikana hata uraia wao wa Tanzania lakini wanaendelea kushiriki katika kuchochea migogoro dhidi ya nchi, akisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kusimama imara kulinda uhuru, amani na mshikamano wa taifa.

Amewataka Watanzania kutokubali mtego wa kubaguana kwa misingi ya kisiasa, kikabila au tofauti nyingine, akieleza kuwa umoja wa kitaifa ndiyo msingi wa maendeleo endelevu na kwamba tofauti za kimtazamo zinapaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo na kuheshimiana.

Sambamba na hilo, ameviomba vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea kuwa macho dhidi ya viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani, huku akiwataka wananchi kushirikiana navyo kwa kutoa taarifa mapema ili kudumisha usalama wa nchi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Tanzania, Marekani zasaini makubaliano ya Dola Bilioni 3.14 kuimarisha sekta ya afya

Serikali za Tanzania na Serikali ya Marekani zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano katika sekta ya afya ya

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu