Mwanamitindo Kylie Jenner pamoja na Rapper Travis Scott Wamebarikiwa KupataMtoto WaPiliPamoja, KupitiaInstagramya Kylie Ametangaza Ujiowa Mtoto Wao Huyo kwa kupost picha iliyoonyesha Mkono umeshikilia mkono wa mtoto mdogo, huku akiweka imoge ya love ya blue nakuandika 2/2/2022.
Ikumbukwe Stormi alizaliwa Februari 1, 2018, Hivyo stormi na Mdogo wake wamezaliwa mwezi mmoja na kupishana tarehe na mwaka tu. Kylie Jenner amethibitisha kuwa mjamzito mnamo Septemba kwamba yeye na rapper Travis walikuwa wanatarajia mtoto wao wapili pamoja.
Mnamo Machi 2019, jarida la Forbes lilimjumuisha Kylie Jenner kwenye orodha ya mabilionea. Jenner alikua bilionea mwenye umri mdogo zaidi duniani akiwa na umri wa miaka 21 utajiriwa Jenner pia unatokana na kampuni yake ya urembo, Kylie Cosmetics, yenye thamani ya dola milioni 800.
