MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

In Kitaifa

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kutoa mchango wao utakaowezesha kuandaliwa Kwa Dira yenye Maono ya Watanzania Kwa Miaka 25 ijayo.

Amezungumza leo jijini Dodoma kuhusu Hafla ya Uzinduzi Wa mchakato Wa maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050,naibu katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango, JENIPHA OMOLO, amesema kuwa ili kufanikisha zoezi la Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kunategemea Kwa kiasi kikubwa ushiriki Wa wadau wote Kwa Maendeleo ya Taifa na watu wake.

OMOLO,amesema serikali ilifanya tathmini ya utekelezaji Wa Dira 2025 kupitia mikakati na programu za Maendeleo ambapo tathmini hiyo ilibainisha uhitaji Wa Taifa kuanza kupanga vipaumbele vya nchi.

Naibu waziri huyo amesema kuwa ,Uzinduzi Rasmi Wa maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 utafanyika tarehe 3 April mwaka huu ambao utafanyika  jijini DODOMA ambapo Watanzania wametakiwa kushiriki  kikamilifu ili kuwezesha kuwa na Dira ya Watanzania.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu