Masau Bwire, Ofisa Habari wa timu ya Ruvu Shooting
amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kosa la
kutoa taarifa za uongo kwenye vyombo vya habari na kauli za
maudhi kwa viongozi wa timu ya Polisi Tanzania FC.
Imeelezwa kuwa taarifa hizo alizitoa katika mchezo uliochezwa
Februari 22, 2020 uwanja wa Ushirika mkoani Kilimanjaro.



