May agonga mwamba mazungumzo mapya Umoja wa Ulaya.

In Kimataifa

Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker amepinga mpango wa Uingereza wa kutaka kufanya mazungumzo mapya juu ya mkataba wa nchi hiyo kujiondoa Umoja wa Ulaya. Bwana Juncker pia amesema wasiwasi juu ya Uingereza kuondoka Umoja wa Ulaya bila ya mkataba umezidi kuwa mkubwa. Akiwahutubia wabunge wa Umoja huo mjini Brussels Juncker pia amepinga kufanyika mazungumzo yoyote mapya juu ya mpaka wa Ireland na amesisitiza kuwa mkataba uliokwishafikiwa kati ya Umoja wa Ulaya na Uingereza ndiyo unaofaa zaidi. Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas amesema mkataba ulioafikiwa ndio unaofaa zaidi na ndio suluhisho la pekee la kuiwezesha Uingereza kuondoka Umoja wa Ulaya. Nchi nyingine za Ulaya pia zimepinga kufanyika mazungumzo mapya juu ya mkataba uliokwishaafikiwa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Tanzania, Marekani zasaini makubaliano ya Dola Bilioni 3.14 kuimarisha sekta ya afya

Serikali za Tanzania na Serikali ya Marekani zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano katika sekta ya afya ya

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu