McGregor atamba kumpasua Mayweather.

In Kimataifa, Michezo

 

Bingwa wa mapigano ya UFC, Conor McGregor ametamba kumsambaratisha aliyekuwa bingwa wa masumbwi ambaye hajawahi kupoteza pambano, Floyd Mayweather baada ya Mamlaka kuridhia matumizi ya ‘gloves’ laini zaidi.

 

Awali, kambi ya Mayweather iliweka masharti kuwa wapiganaji hao watatumia gloves zenye vipimo vya 10oz, lakini Nevada State Athletic Commission (NAC) imeridhia matumizi ya gloves zenye vipimo vya 8oz.

 

McGregor amesema kuwa kwakuwa gloves zimekuwa laini zaidi basi atakuwa na uwezo wa kumaliza pambano lao ndani ya raundi mbili.

 

“Siamini kama kwa kutumia gloves zenye vipimo hivi laini zaidi ataweza kuvuka raundi ya pili,” McGregor mwenye umri wa miaka 29 alitamba.

 

“Ningependa kuonesha ujuzi na uwezo wa kumpiga lakini sioni kama atakuwa na uwezo wa kuvumilia masumbwi yangu,” aliongeza.

 

Mbabe huyo aliongeza kuwa yuko tayari kwa pambano la raundi 12 dhidi ya Mayweather lakini anaamini kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kulimaliza pambano mapema.

 

McGregor amezoea kutumia gloves zenye ukubwa wa 4oz kwenye mapambano ya UFC, na Mayweather amewahi kutumia gloves zenye ukubwa wa 8oz kwenye mapambano yake 46 kati ya 49.

 

Hata hivyo, wadau wengi wa masumbwi ikiwa ni pamoja na bondia Manny Pacquiao na Mike Tyson hawampi nafasi yoyote McGregor hata kuonesha ushindani wa maana dhidi ya Mayweather ambaye ni mzoefu na bingwa wa mchezo huo.

 

Pambano hilo linalotarajiwa kuvunja rekodi ya kutengeneza kiasi kikubwa zaidi cha fedha litafanyika Agosti 26 mwaka huu nchini Marekani.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKAGUA BARABARA YA SOMANGA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa asubuhi ya leo  Aprili 16, 2025 amewasili eneo la Somanga kukagua Miundombinu ya barabara kuu

Read More...

HATUTAWAACHIA CCM NAFASI TUTASHIRIKI UCHAGUZI MKUU – ACT WAZALENDO

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu amesema chama hicho kitashiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka

Read More...

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamohanga Afariki Dunia 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Gissima Nyamohanga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika ajali

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu