Rais wa Marekani aliamua Jumanne hii usiku kutia saini amri ya kupitia upya mpango wa kudhibiti utoaji wa visa za kazi kwa wageni nchini Marekani maarufu kama H-1B. Lakini bunge la Congress litakabiliwa na kibarua kigumu kwa kupitisha sheria hiyo. Wabunge ndio wana uwez0 wa kuidhinisha au la sheria hiyo.
Rais Trump alichagua jimbo la Wisconsin, ambalo linakabiliwa na mdororo wa kiuchumi,akiomba kuwekeza katika jimbo hilo na kuajiri kwanza raia wa Marekani kabla ya mtu yeyote. Alitoa hotuba yake mbele ya bendera ya American katika jimbo la Wisconsin.
Sheria hii inayataka mashirika kufuata taratibu za Serikali katika kuondoa wafanyakazi wa kigeni kwenye mpango wa kuwania zabuni kwenye miradi ya serikali.
Sheria hii ina nia ya kutimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa Kampeni ya ”Marekani kwanza”.
Trump atatoa maelekezo kwa idara ya mambo ya ndani, sheria, usalama wa ndani na kazi na kupendekeza kufanyia mabadiliko mpango huo, ambao unawaruhusu waajiri nchini humo kuwapa wageni nafasi za kazi.
