Mwanajeshi auawa Afrika ya kati.

In Kitaifa

Mwanajeshi mmoja wa kulinda amani kutoka Tanzania ameuawa, katika shambulio lililotokea Jamhuri ya Afrika ya Kati na walinda amani wengine 7 wamejeruhiwa.

Shambulio hilo limetekelezwa dhidi ya kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa wakati kikiwa kwenye doria katika Kijiji cha Dilapoko kilichopo Kusini Magharibi mwa Mji wa Mambere-Kadei.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric amesema inaaminika kuwa shambulio hilo limetekelezwa na wapigani wa Kikundi cha Siriri.

Kati ya waliojeruhiwa mmoja yuko katika hali mbaya anaendelea kutibiwa katika hospitali ya Bangui huku wengine watatu wakiendelea na matibabu katika mji wa Berberati.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu