Polepole alinyatia Jimbo la Buyungu.

In Siasa
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Ndg. Humphrey Polepole amewaonya Vongozi wa vyama vya Upinzani nchini, Mbowe pamoja na Zitto Kabwe baada ya kukubaliana kushirikiana kumpata Mbunge jimbo la Buyungu lililoachwa wazi na Mwl. Kasuku Bilago kwa kuwaambia wembe wa CCM ni ule ule.
Polepole amesema hayo ikiwa zimepita siku kadhaa baada ya mazishi ya Mwl. Kasuku Bilago kuzikwa huko Kakonko mkoani Geita baada ya kuugua kwa muda mfupi na kisha kwenda kuzikwa huko kijijini kwao.
Polepole amesema kuwa “Nimesikia jamaa palepale msibani walianza kugawana ubunge na kuanza kujihadaa, ni bahati mbaya sana. Utamaduni wa kiafrika ni kumaliza msiba ambapo lengo ni kufariji wafiwa”.
Ameongeza kuwa “Nimekaa Kakonko kwa muda wa kutosha, kwakuwa mmeanza siasa msibani, CCM tunasema wembe ni uleule”.
Wakiwa kwenye mazishi ya Mwalimu Bilago ambaye alikuwa Mbunge kupitia CHADEMA, Zitto Kabwe pamoja na Mbowe walikubaliana kuweka umoja ambao utamsimamisha mgombea mmoja anayekubalika kutoka upinzani na kuhakikishia wanampigania hadi anashinda ili kumuenzi mwalimu

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu