Rais Samia atoa onyo mkoa wa Dar es salaam

In Kitaifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametoa onyo kwa vitendo vya ujambazi vilivyoanza kujitokeza jijini Dar es salaam.

Amesema hayo leo Mei 7, 2021 alipoongea na wazee wa Dar es salaam katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

”Nimesoma mtandaoni Dar kuna watu wanajaribu kupima kina cha maji, viujambazi vimeanza kuja juu, naomba nitoe meseji wasijaribu kina cha maji, IGP upo hapa, mitandaoni wanamtaja afande mmoja alikomesha ujambazi, wanasema Mama turudishie” – Rais Samia Suluhu.

Aidha Rais Samia amesema huko mbeleni kwenye kujenga uchumi wa nchi atateua watu kwa kufuata welefi na si itikadi za vyama vyao.

”Katika kupanga safu za kujenga uchumi sitochagua, mtanzania yeyote mwenye weledi na umahiri anayeweza kuleta manufaa kwa Taifa nitamuingiza afanye kazi, sitochagua huyu katoka chama kipi yule katoka chama gani, lengo letu ni kujenga umoja wa watanzania” – Rais Samia Suluhu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu