Mkuu wa mkoa wa mbeya Mhe. Comrede Juma Zuberi Homera amefanya uzinduzi wa wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya Taifa (NIDA) huku akiwataka wakuu wa wilaya wote kufanya uzinduzi huo kwenye wilaya zao.


Uzinduzi huo umefanyika Novemba 27/2023 katika kata ya Isuto halmashauri ya wilaya mbeya huku ukishuhudiwa na viongozi mbali mbali wa halmashauri hiyo akiwemo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Mbeya Vijijini Ndg. Ackimu Sebastiani Mwalupindi.
Mhe. Comrade Homera katika uzinduzi huo pia amewasisitiza viongozi wa kata kuhakikisha wanagawa vitambulisho hivyo vyote kwa wahusika kwani wananchi wamekuwa wakivisubiri kwa muda mrefu.
Hata hivyo Comrade amesema amemshukuru Rais Dkt. Samia kwakuwapatia vitambulisho hivyo zaidi ya 360,000 katika mkoa wa mbeya huku halmasya wilaya ya Mbeya ikiongoza kupata vitambulisho vingi.
