Serikali katika mwaka wa fedha 2017/18, imetenga Sh bilioni 56 kwa ajili ya kufanya ukarabati majengo na mabweni katika vyuo vikuu mbalimbali nchini.

In Kitaifa

Serikali katika mwaka wa fedha 2017/18, imetenga Sh bilioni 56 kwa ajili ya kufanya ukarabati majengo na mabweni katika vyuo vikuu mbalimbali nchini.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Stella Manyanya alisema ukarabati huo utahusisha pia majengo ya Chuo Kikuu Mzumbe, Morogoro. Manyanya alisema ameshatoa ushauri kwa viongozi wa chuo hicho kuhakikisha wanatumia fedha za ndani kuhakikisha wanafanya ukarabati wa miundombinu ya maji katika chuo hicho.

Amesema pia ukarabati huo utaenda sambamba na ujenzi wa bweni la Chuo Kikuu Huria (OUT) Dodoma, ukarabati wa majengo ya Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara Moshi (MUCCOBS), ujenzi wa mabweni uliofanyika Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kishiriki cha Elimu (Duce).

Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Asha Juma (CCM) aliyetaka kujua kuna utaratibu gani wa kuyafanyia ukarabati majengo ya Chuo Kikuu Mzumbe Morogoro, Manyanya alisema serikali imeanza ukarabati wa miundombinu na majengo katika kampasi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro kwa gharama ya Sh bilioni mbili.

Amesema hadi kufikia Mei 31 mwaka huu, Sh milioni 884.6 zilizotengwa zilikwishatolewa na wizara na inaendelea kufuatilia hizo zilizobaki ili zitolewe kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha.

Amesema kwa juhudi hizo za ukarabati unaoendelea kutekelezwa chuoni hapo ni dhahiri serikali ina nia ya dhati ya kuinua hadhi ya chuo hicho, kuweka mazingira stahiki ya kufundishia na kujifunzia pamoja na kuwapunguzia adha wasichana .

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu