Sugu anyimwa dhamana arudishwa rumande.

In Kitaifa
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyassa, Emmanuel Masonga wamerudishwa rumande hadi Januari 22, 2018 siku ya Jumatatu ambapo kesi yake itaanza kusomwa mfululizo.
Mbunge huyo wa Mbeya mjini na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyassa wanashikiliwa na jeshi la polisi wakituhumiwa kutenda kosa la uchochezi katika mkutano wao wa hadhara ambao ulifanyika Disemba 31, 2017 jijini Mbeya ambapo jeshi la polisi linasema kuwa viongozi hao walizungumza maneno yenye kuleta chuki kati ya Serikali na wananchi.
Mchana wa January 16, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini Mbeya iliamuru Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyassa Emmanuel Masonga wapelekwe rumande mpaka January 19 ambayo ni leo kwa kesi ya uchochezi.
Viongozi hao wamerudishwa rumande tena mpaka siku ya Jumatatu ambapo kesi yao itaanza kusomwa tena

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu