Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la kuhamasisha matumizi salama ya barabara na kuboresha usalama wa waendesha bodaboda nchini.
Ushirikiano huo uliozinduliwa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Unywaji Bia kwa Uwajibikaji (Global Responsible Beer Day), unalenga kukabiliana na ongezeko la majeruhi na vifo vinavyotokana na ajali za bodaboda kupitia elimu, mafunzo, uhamasishaji na utetezi wa usalama barabarani, huku ukichangia kujenga jamii salama na zenye afya bora.
Usafiri wa bodaboda ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya ajali za barabarani nchini Tanzania, hususa ni katika maeneo ya mijini kama Dar es Salaam. Licha ya kuwepo kwa sheria za usalama barabarani, changamoto kama matumizi ya kofia ngumu kwa abiria, uendeshaji usiozingatia usalama, kutofuata sheria za usalama barabarani pamoja na kuwepo kwa madereva chini ya miaka 18 na waendesha vyombo vya moto wasio na mafunzo . Hizi ni miongoni ya sababu zinapelekea kuwepo na uhatarishi wa maisha ya watumiaji wa barabara kila mwaka.
Kupitia ushirikiano huo, TBL na Tanzania Red Cross Society zitafanya kazi kwa pamoja kuhamasisha mabadiliko ya kujenga utamaduni wa uwajibikaji miongoni mwa waendesha bodaboda na abiria.
Akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Masuala ya Mahusiano wa TBL, Bi. Neema Temba, alisema kampuni hiyo inaamini kuwa kujenga jamii imara kunakwenda sambamba na kuhakikisha usalama na ustawi wa wananchi.
“Katika Kampuni ya TBL, tunaamini kuwa kujenga jamii zinazostawi kunakwenda sambamba na kuhakikisha usalama na ustawi wa wananchi wake. Kupitia kampeni yetu ya Cheers to Moderation, tunahamasisha watu kufanya maamuzi yenye uwajibikaji, si katika matumizi ya bidhaa pekee, bali pia katika maisha yao ya kila siku.
“Usalama barabarani ni suala linalohusu jamii nzima kwa sababu huathiri familia, shughuli za kujipatia kipato na mustakabali wa taifa letu. Ushirikiano huu na Tanzania Red Cross Society unaonesha dhamira yetu ya kujenga mazingira salama kwa jamii tunazozihudumia kupitia kuhamasisha uendeshaji salama, kuongeza uelewa na kusaidia kuokoa maisha ya watu barabarani,” alisema Temba.
Mpango huu wa Bodaboda 1600 kiujumla unatekelezwa kwa kuzingatia maeneo makuu matatu:
1. Kuhamasisha utii wa sheria za usalama barabarani
Kushirikiana na wadau husika, wakiwamo mamlaka za usalama barabarani na wasimamizi wa sekta hiyo, ili kuhamasisha uzingatiaji wa sheria na kanuni za uendeshaji (boda boda) salama.
2. Uhamasishaji na Mawasiliano
Kupitia eneo hili, kampeni maalumu za uhamasishaji zitaendeshwa zikilenga matumizi ya kofia ngumu, umri unaoruhusiwa kisheria kuendesha bodaboda, uzingatiaji wa sheria za usalama barabarani na tabia zinazofaa kwa madereva.
3. Elimu na Mafunzo:
Kutoa elimu na mafunzo ya usalama barabarani yatakayolenga kuongeza maarifa na uwezo wa waendesha bodaboda kuhusu kanuni za usalama barabarani, alama za barabarani na namna sahihi ya kuendesha bodaboda.
Ushirikiano huo unaonesha dhamira ya TBL ya kuchangia maendeleo endelevu ya jamii na kutekeleza wajibu wake kama kampuni inayowajibika kwa jamii.
Kwa upande wake Bwana. Reginald Mhango – Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taasisi (Tanzania Red Cross Society) alisema dhamira ya taasisi ni kulinda maisha na kuimarisha uwezo wa jamii kukabiliana na changamoto mbalimbali.
“Dhamira kuu ya Tanzania Red Cross Society ni kulinda maisha na kuimarisha uwezo wa jamii kukabiliana na majanga. Kila siku tunashuhudia madhara makubwa yanayosababishwa na ajali za barabarani na kuepelekea kupoteza maisha ya watu na wakati mwingine kusababisha ulemavu wa maisha. Ushirikiano huu na Kampuni ya TBLTanzania ni hatua muhimu katika kukabiliana na mojawapo ya sababu kuu za majeraha na vifo vinavyoweza kuzuilika miongoni mwa waendesha bodaboda. Kwa kuunganisha nguvu katika uhamasishaji, elimu, ushirikishwaji wa jamii na utetezi, tunalenga kuhimiza tabia salama barabarani na kuhakikisha watu wengi zaidi wanarejea nyumbani salama kwa wapendwa wao,” alisema.
Waendesha bodaboda wana nafasi muhimu katika kuwaunganisha wananchi, kusaidia shughuli za biashara na kurahisisha upatikanaji wa maeneo ya kazi, shule, masoko na huduma za afya.
Kwa kuwekeza katika elimu na uhamasishaji wa usalama barabarani, mpango huo unalenga kulinda madereva, abiria, watembea kwa miguu na familia zinazokumbwa na madhara ya ajali za barabarani.
Kila maisha yanayopotea au mtu kupata majeraha makubwa kutokana na ajali za barabarani huathiri si mtu mmoja pekee, bali pia familia na jamii nzima.
Kupitia juhudi za pamoja, mpango huo unalenga kuchangia upatikanaji wa barabara salama, jamii imara na kujenga utamaduni wa matumizi sahihi ya barabara kuwa jukumu la kila mmoja.
Akizungumzia ushirikiano huo, mwakilishi wa Tanzania Red Cross Society alisisitiza kuwa majeraha yanayotokana na ajali za barabarani bado ni changamoto kubwa ya afya ya umma. Alieleza umuhimu wa ushirikiano unaounganisha uhamasishaji wa jamii, elimu na utetezi katika kuokoa maisha na kuimarisha uwezo wa jamii kukabiliana na changamoto hizo.
Katika utekelezaji wa mpango huo, ujumbe mkuu wa kampeni utajumuisha:
• Hakuna kofia ngumu ya kujikinga, hakuna safari (No Helmet, No Ride).
• Miaka 18 na kuendelea tu. Umri halali wa kuendesha bodaboda huokoa maisha (18+ Only. Legal Riding Age Saves Lives).
• Usalama unaanzia kwako (Safety Starts with You).
• Mlinde abiria wako, linda maisha yako ya baadaye (Protect Your Passenger, Protect Your Future).
Kupitia juhudi hizo, mpango unalenga kuongeza uelewa kuhusu sheria za usalama barabarani, kuimarisha uzingatiaji wa kanuni za usalama, kupunguza tabia hatarishi za uendeshaji na hatimaye kupunguza majeraha na vifo vinavyotokana na ajali za bodaboda kwa muda mrefu.
Ushirikiano huo pia unaendana na dhamira ya Siku ya Kimataifa ya Unywaji Bia kwa Uwajibikaji, inayohamasisha watu binafsi na taasisi kufanya maamuzi yenye uwajibikaji yanayochangia kujenga jamii salama na zenye afya bora.
Kuhusu mpango huo
Mpango wa Usalama Barabarani kwa Bodaboda unatekelezwa kupitia kampeni ya TBL ya Cheers to Moderation. Unalenga kuhamasisha matumizi sahihi ya barabara na kuboresha usalama wa jamii kupitia elimu, uhamasishaji, mafunzo na ushirikiano na wadau mbalimbali.
Mpango huo unaimarisha dhamira ya TBL ya kuendesha biashara kwa uwajibikaji na kuleta matokeo chanya katika jamii kwa kusaidia kujenga mazingira salama, yenye afya bora na jamii zinazoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali nchini Tanzania.
MWISHO



