Zaidi ya watu 800 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 1,300 kujeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi la ukubwa wa 6.0 katika kipimo cha Ritcher lililotokea Jumapili jioni nchini Afghanistan.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Taliban, tetemeko hilo limeathiri miji kadhaa katika jimbo la Kunar, karibu na mji wa Jalalabad, na kusababisha uharibifu mkubwa wa makazi. Waziri wa Mambo ya Ndani, Abdul Matin Qani, ameliambia shirika la habari la AP kuwa vifo na majeruhi pia yamerekodiwa katika jimbo jirani la Nangarhar, huku nyumba nyingi zikiripotiwa kuanguka.
Mkazi wa wilaya ya Nurgal eneo lililoathirika zaidi—amesema karibu kijiji kizima kimeporomoka na watu wakiwemo watoto na wazee wamefukiwa na vifusi.



