TTCL kuwafikia Vijijini.

In Tekinolojia

Shirika la simu Tanzania Tccl kanda ya kaskazini imeweka mikakati maalumu ya kuifikia jamii ili waweze kuwaelewa zaidi kwa kutumia huduma hiyo.


Huduma za sauti pamoja na huduma za internet kwa viwango ambavyo vina unafuu zaidi na vyenye ubora
Akizungumza na vyombo vya habari Afisa Masoko na Mauzo katika shirika hilo Bw Fredrick Manyala amesema kuwa wanatoa huduma hizo kwa kulenga wananchi wale ambao hawana uwezo wa kufikia huduma za mawasiliano ambapo hivi karibuni wamezindua mnara kijiji cha Mundarara Kilichopo wilaya ya Longido Mkoani Arusha

Lengo la shirika na mikakati yake ni kuweza kuwafikia wananchi wote ambapo kuna vifurushi mbalimbali kama longer park, ambapo bei zake ni nafuu na kinatoa dakika nyinyi za maongezi mwezi dk60, dak 100 kwa shilingi elfu 3 dakika 200 shilingi elfu tano mitandao yote, na dakika 400 elfu kumi ndani ya mwezi mmoja, na dakika 850 kwa shilingi elfu 20 ndani ya mwezi.


Amesema kuwa mikakati ambayo wameweka ni pamoja na kuwafikia wananchi hasa wa vijijini kwa kutumia vifurushi mbalimbali kikiwemo cha wiki, na mwezi na kujua namna ya kutumia line za TTCL.


“Watanzania waliunge mkono shirika la mawasiliano Tanzania kwa sababu ni shirika la watu wote na watu wahakilishe wanasajili laini zao kwa alama za vidole” alisema Fredrick

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WATANZANIA WATAKIWA KUIUNGA MKONO JKT QUEENS

MKUU wa JKT Meja Jenerali RAJABU MABELE, amewataka watanzania kuiunga mkono timu ya JKT Queens inayokwenda kuliwakilisha Taifa na

Read More...

SERIKALI YATOA BIL 424.6 UTEKELEZAJI MIRADI YA TANRODS RUKWA-ENG MWANGA

KATIKA kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu