Waziri mkuu wa Ukraine ajiuzulu

In Kimataifa

Waziri Mkuu wa Ukraine Oleksiy Honcharuk amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa mara ya pili katika miezi miwili. Wabunge kutoka chama tawala wataamua leo kama watakubali kujiuzulu kwake au la wakati wa kikao maalum. Waziri wa fedha na mambo ya nchi za kigeni huenda pia wakaondolewa katika nyadhifa zao kama sehemu ya mabadiliko ya baraza la mawaziri. Naibu Waziri Mkuu Denys Shmygal anapigiwa upatu kuchukua nafasi ya Honcharuk. Shmygal awali alihudumu kama mkuu wa utawala wa kikanda katika jimbo la magharibi la Ivano-Frankvisk kabla ya kuchukua wadhifa wa naibu waziri mkuu mwezi uliopita. Hakukuwa na kauli ya mara moja kutoka kwa Honcharuk au Rais Volodymyr Zelenskiy. Haijafahamika wazi kilichomfanya Honcharuk kuwasilisha barua ya kujiuzulu kwa mara ya pili.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Tanzania, Marekani zasaini makubaliano ya Dola Bilioni 3.14 kuimarisha sekta ya afya

Serikali za Tanzania na Serikali ya Marekani zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano katika sekta ya afya ya

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu